Home news KUELEKEA MECHI YA SHIRIKISHO JUMAPILI…WAARABU WAIJIA SIMBA KIBABE…WAPANDA DEGE LA KIFAHARI…

KUELEKEA MECHI YA SHIRIKISHO JUMAPILI…WAARABU WAIJIA SIMBA KIBABE…WAPANDA DEGE LA KIFAHARI…


Kikosi cha RS Berkane kimeanza safari ya kuelekea Dar es salaam Tanzania, tayari kwa mchezo wa Mzunguuko wa 04 wa ‘Kundi D’ Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Simba SC.

Mchezo huo utapigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam Jumapili (Machi 13), huku Simba wakiweka dhamira ya kuendeleza rekodi yao kufanya vizuri kwenye Uwanja huo.

Katika mchezo wa Mzunguuko wa 03 uliopigwa mjini Berkane-Morocco Frebruari 27, Simba SC ilikubali kufungwa mabao 2-0.

Picha za baadhi ya wachezaji wanaounda kikosi cha RS Berkane zimewekwa kwenye ukurasa wa Instagram wa klabu hiyo.

RS Berkane inongoza msimamo wa ‘Kundi D’ ikiwa na alama 06, ikifuatiwa na Simba SC ya Tanzania yenye alama 04 sawa na USGN ya Niger huku ASEC Mimosas ya Ivory Coast ikiwa na alama 03.

SOMA NA HII  MTIBWA WAJIWEKA KANDO ISHU YA ABDI BANDA KUICHAFUA SIMBA AFRIKA KUSINI...AIPAKA MATOPE KINOMA...