Home Namungo FC KUHUSU KELELE ZA WANAOMSEMA KUWA HANA STAILI YA KUSHANGILIA …LUSAJO AWAJIBU HIVI...

KUHUSU KELELE ZA WANAOMSEMA KUWA HANA STAILI YA KUSHANGILIA …LUSAJO AWAJIBU HIVI ‘KIBABE’..


Mshambuliaji wa Namungo FC Reliant Lusajo amewajibu baadhi ya Wadau wa Soka la Bongo ambao wamekua wakihoji ubunifu wa ushangiliaji pale anapoifungia timu yake kwenye Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Hoja hiyo iliibuka kufuatia Lusajo kukosa aina ya Ushangiliaji ambayo haiwavutii mashabiki wa soka, kama ilivyo kwa mshindani wake kwenye orodha ya kufumania nyavu msimu huu Mshambuliaji wa Young Africans Fiston Kalala Mayele.

Mshambuliaji huyo mzawa amesema anashangazwa kuona watu wakihoji aina ya ushangiliaji wake, kitu ambacho kwake hakina msingi katika soka lake, zaidi ya kuisaidia Namungo FC kufikia lengo la kufanya vizuri kila inapokua Uwanjani.

Amesema: “Mbona kuna mastaa wa nje wanashangilia kwa aina yoyote inayowajia wakati huo kama mimi tu”

“Sina mpango wa kushindana na hilo, natamani kufunga zaidi”

Wadau wa Soka la Bongo walimtaka Lusajo kubuni aina ya kushangilia itakayovutia ili kujiwekea mazingira ya kuzungumzwa sana kama ilivyo kwa Mayele.

Wawili hao hadi sasa wameshazifumania nyavu mara 10 kwa kila mmoja, katika michezo 17 ya Ligi Kuu waliyocheza, huku Lusajo akiwa na nafasi nyingine ya kuongeza bao leo Jumatano (Machi 16), endapo ataifunga Azam FC kwenye mchezo utakaopigwa Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi.

SOMA NA HII  BAADA YA KUIPAISHA SIMBA KIMATAIFA...GOMES AFANYA KWELI ...AWAPA UBINGWA WAAABU...