Home Habari za michezo BAADA YA INONGA KUMNYANYASA MAYELE JUZI…MASHABIKI SIMBA WAFANYA YAO HUKO…

BAADA YA INONGA KUMNYANYASA MAYELE JUZI…MASHABIKI SIMBA WAFANYA YAO HUKO…


Beki wa Kati kutoka DR Congo Henock Inonga Baka ametajwa kuwa mshindi wa Tuzo ya mchezaji bora wa Mashabiki wa Simba SC kwa mwezi April 2022.

Simba SC kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii imemtangaza Beki huyo kuwa mshindi, akiwashinda wachezaji wenzake wanaocheza nafasi ya ulinzi Shomari Kapombe na Joash Onyango.

Taarifa iliyochapishwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii ya Simba SC imeeleza: “🏅Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki (Emirate Aluminium Simba ACP Fans Player of the Month) mwezi Aprili inakwenda kwa Henock Inonga 👏 #NguvuMoja”

Inonga alionesha kiwango cha hali ya juu katika michezo ya Simba SC kwa mwezi April, hatua ambayo ilimsukuma kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho.

Wakati huo huo kikosi cha Simba SC kimerejea jijini Dar es salaam mapema leo Jumatano, kikitokea Lindi kupitia Mtwara.

Simba SC jana iliambulia matokeo ya sare ya 2-2 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa mzunguuko wa 22 wa Ligi Kuu uliopigwa Uwanja wa Ilulu mjini Lindi.

SOMA NA HII  CHEZA BUREE NA USHINDE KUPITIA CASINO ZA MERIDIANBET....