Home news RASMI…”MCHAWI MWEUSI’ KUTOKA AFRIKA KUSINI PITSO MOSIMANE APATA ‘SHAVU’ JIPYA AL AHLY…WAARABU...

RASMI…”MCHAWI MWEUSI’ KUTOKA AFRIKA KUSINI PITSO MOSIMANE APATA ‘SHAVU’ JIPYA AL AHLY…WAARABU WANUNA..


Kocha Mkuu wa Klabu ya Al Ahly ya Misri, Pitso Mosimane (57) raia wa Afrika Kusini ameongeza mkataba mpya wa miaka miwili wa kuendelea kuitumikia timu hiyo hadi msimu wa mwaka 2023/24.

Mosimane alitangazwa rasmi kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo Oktoba mwaka 2020 akitokea ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Taarifa hii imethibitishwa na Al Ahly wenyewe ambao kupitia kurasa zao za kijamii na tovuti wametangaza juu ya mkataba huo mpya ambapo pia wasaidizi wa kocha huyo nao wameongeza mkataba wa miaka miwili.

Awali ilikuwa ikiaminika kocha huyo atafukuzwa au kuondoka klabuni hapo baada ya mkataba wake kuwa unaelekea ukingoni, wakongwe kadhaa wa Al Ahly waliowahi kucheza kikosini hapo na wachambuzi wa Misri walikuwa wakimshutumu kuwa hana uwezo wa kuifundisha timu hiyo.

SOMA NA HII  MKATA UMEME WA SINGIDA BIG STAR 'AIWANGIA' SIMBA MECHI YAO YA KESHO...