Home news RASMI..NABI AAMUA KUMWEKA KANDO ‘SURE BOY’ KWENYE KIKOSI CHAKE…SABABU HIZI HAPA…

RASMI..NABI AAMUA KUMWEKA KANDO ‘SURE BOY’ KWENYE KIKOSI CHAKE…SABABU HIZI HAPA…


KIUNGO mchezeshaji fundi ndani ya Yanga SC, Salum Aboubakary ‘Sure Boy’ ameondolewa kwenye mipango ya mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC.

Machi 16, mwaka huu, Yanga inatarajiwa kucheza dhidi ya KMC, mechi ya Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kupigwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Sure Boy ambaye alijiunga na Yanga katika usajili wa dirisha dogo msimu huu, ameonekana kuwa na kiwango bora eneo la kiungo ambalo pia linachezwa na Khalid Aucho, Yannick Bangala, Feisal Salum ‘Fei Toto’ na Zawadi Mauya.

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, alisema atamkosa kiungo huyo katika mchezo dhidi ya KMC kutokana na adhabu ya kadi tatu za njano alizonazo.

Nabi alisema kiungo huyo amefikisha kadi hizo tatu ambazo amezipata kwenye mechi za ligi dhidi ya Mtibwa Sugar, Biashara United na Geita Gold.

Aliongeza kuwa, licha ya kumkosa kiungo huyo, lakini wapo wengine wenye viwango bora watakaochukua nafasi yake akiwemo Mganda, Khalid Aucho.

“Sure Boy hatakuwa sehemu ya kikosi changu

kitakachocheza dhidi ya KMC, hiyo ni kutokana na adhabu ya kadi tatu za njano alizozipata katika michezo iliyopita ya ligi.

“Wakati Sure Boy akiukosa mchezo huo, Aucho anatarajiwa kurejea kikosini baada ya afya yake kuimarika zaidi, kumbuka aliukosa mchezo uliopita wa ligi kutokana na kuwa majeruhi.

“Hivyo sina hofu kukosekana kwake, wapo wengine watakaochukua nafasi yake, ninafurahia kuona baadhi ya majeruhi wakirejea baada ya kupona akiwemo Aucho, Said Ntibazonkiza, Shabani (Djuma) na Ushindi (Chico),” alisema Nabi.

SOMA NA HII  ISHU YA MORRISON, CAS YAOMBA SAMAHANI