Home Habari za michezo UKWELI NI KWAMBA..MORRIOSN NI MCHEZAJI FULANI WA MCHONGO MCHINGO HIVI…BASI TU YANI…

UKWELI NI KWAMBA..MORRIOSN NI MCHEZAJI FULANI WA MCHONGO MCHINGO HIVI…BASI TU YANI…


KUNA nyakati tunaishi katika maigizo kuliko uhalisia. Ni kama nyakati hizi za Bernard Morrison. Mchezaji fulani hivi wa mchongo ambaye amepata jina kubwa kwenye soka la Tanzania kuliko uhalisia.

Tanzania kuna nyakati inaishi maisha ya peke yake. Hii ndiyo sababu Morrison ameweza kupanda mpira kisha akapanda pia na vichwa vya watu. Halafu hakuna anayejali.

Ligi Kuu ya Tanzania Bara imewahi kuwa na wachezaji wengi mahiri. Walikuwepo wengi zamani kama kina Zamoyoni Mogela, Sekilojo Chambua, Edibily Lunyamila, Abeid Mziba, Dua Said, Said Mwamba Kizota, Athuman China na wengineo. Walikuwa wachezaji kwelikweli.

Baadaye wakaja kina Yusuph Macho, Emmanuel Gabriel na wengineo. Kisha wakaja hawa kina Mussa Hassan ‘Mgosi’, Mrisho Ngassa, Kipre Tcheche na wengine wengi. Hawa walikuwa wanaume wa shoka. Sifa zao na kazi zao uwanjani zilifanana.

Yule Mrisho Ngassa katika ubora wake aliwahi kuwa mfungaji bora wa Ligi ya Kuu ya Tanzania Bara. Yule Kipre Tcheche katika ubora wake alikuwa mfungaji bora na mchezaji bora wa Ligi ya Tanzania.

Ni kama ilivyotokea baadaye kwa Emmanuel Okwi. Mchezaji mmoja wa maana kutoka pale Uganda. Alikuwa na jina kubwa nje ya uwanja, lakini katika kila mechi angekuwa kitu cha kujivunia.

Lakini siku hizi mpira umekuwa kitu cha ajabu. Mchezaji kama Morrison ana jina kubwa lakini uwanjani anakupa nini? Mchezaji ambaye hajawahi kufikisha magoli matano kwa msimu mmoja. Mchezaji ambaye akicheza vizuri leo, ni mpaka usubiri sana.

Ubaya ni kwamba Morrison alisajiliwa na Simba kisiasa na kwa miaka miwili hajafanya chochote cha maana. Hivyo huenda akaendelea kuwepo Simba zaidi na zaidi licha ya kuwa hafanyi lolote la maana. Ni mchezaji wa mchongo tu.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA WAMOROCCO...SIMBA WAULINDA USIKU NA MCHANA UWANJA WA MKAPA...ISHU IKO HIVI...