Habari za michezo

KWA MWENDO HUU YANGA LAZIMA AWE BINGWA ‘JAMENI’…WAUKARIBISHA MWEZI MTUKUFU ‘KISTAILI’…

admin April 1, 2022 6:30 pm


Wachezaji na Benchi la Ufundi la Young Africans leo Ijumaa (Aprili Mosi) wametoa misaada kwa vituo mbalimbali vya Watoto Yatima vya jijini Dar es salaam.

Young Africans wametoa misaada hiyo, ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Shughuli hiyo imesimamiwa na Wadhamini na Wafadhili wa klabu hiyo Kongwe katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati Kampuni ya GSM, ambayo imekua mstari wa mbele hasa msimu huu kufanikisha lengo la kurejesha kwa jamii.

Mbali na kutoa msaada pia Watoto wanaolelewa kwenye vituo hivyo walipata muda wa kucheza pamoja na wachezaji na viongozi wa Young Africans katika viwanja vya Gymkhana.

KISA MIKATABA MIPYA KWA WACHEZAJI..NABI AWACHIMBA ‘MKWARA WA KUFA MTU’ YANGA… BAADA YA KUONA WANAZIDI KUPOTEANA…DIRK KUYT WA LIVERPOOL AWACHAGULIA MAN UTD KOCHA MPYA..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply