Habari za michezo

PABLO NA CHAMA WAIKUNG’UTA YANGA TUZO ZA MWEZI MACHI…NABI ‘ATIMULIWA VUMBI JEUSI’…

admin April 6, 2022 11:25 am


Kiungo wa Simba Clatous Chota Chama amefanikiwa kuibuka mchezaji bora wa mwezi Machi Ligi Kuu Tanzania Bara, NBC Primia Ligi.

Wakati Chama akiibuka mchezaji Bora, Kocha wa Simba Pablo Franco Martin amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa Mwezi Machi Ligi Kuu Bara.

Chama ameibuka kidedea akiwapiku Fiston Mayele wa Yanga na Frank Kahole wa Mtibwa Sugar.

Kwa mwezi Machi, Chama amecheza michezo miwili na kufunga magoli mawili huku michezo yote miwili wakiibuka na ushindi.

Kwa Upande wa Kocha Pablo amewagaragaza Nasreddine Nabi wa Yanga na Francis Baraza wa Kagera Sugar baada ya kufanikiwa kuingoza Simba kushinda michezo yake miwili dhidi ya Biashara United na Dodoma Jiji.

Mbali na hao tuzo ya Meneja Bora wa Uwanja imekwenda kwa Gordon Nsajigwa, Meneja wa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

MANARA AWAITA ORLANDO PIRATES…'”NJOONI WANAUME…WANANCHI WEZENU TUPO…. KUELEKEA MECHI YA LEO…TAKWIMU ZINAONGEA….YANGA WAIZIDI AZAM KIDOOGO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply