Habari za michezo

SIMBA NA NAMUNGO ZAMTIA WAZIMU NABI…AWACHARUKIA WACHEZAJI MAZOEZINI LEO…

admin April 15, 2022 2:29 pm


KOCHA Mkuu wa Yanga Mtunisia, Nasreddine Nabi amewapiga mkwara mastaa wake kwa kuwataka kutofikiria mchezo wa Dabi ya Kariakoo na badala yake kuhamisha akili zao dhidi ya Namungo FC.

Yanga kabla ya kuvaana dhidi ya Simba Aprili 30, mwaka huu katika Dabi ya Kariakoo watacheza dhidi ya Namungo Aprili 24, katika mchezo wa ligi kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Timu hiyo tayari ipo kambini tangu wiki iliyopita ikijiandaa na michezo ya ligi ambao wiki iliyopita walifuzu hatua ya Robo Fainali ya Kombe la FA kwa kuwaondoa Geita Gold kwa njia ya penalti.

Yanga iko kwenye maandalizi kambini Kijiji cha Avic Town, Kigamboni nje kidogo ya Dar ni kwa ajili ya Namungo na siyo Simba.

Nabi alisema: “Michezo yote miwili iliyokuwepo mbele yetu ni muhimu ambayo itatupa pointi tatu kila mmoja, hivyo ngumu kwa wachezaji wangu kuudharau mchezo dhidi Namungo.

“Tunaanza na Namungo kwanza kuchukua pointi tatu, baada ya hapo wanafuatia Simba, hivyo siufikirii kabisa mchezo wa dabi kwa hivi sasa.”

WAKATI WAKIJIANDAA NA WASAUZI KESHO KUTWA….SIMBA WAIPA YANGA SIKU 5 TU…AHMED ALLY AWANANGA.. STRAIKA HATARI WA ORLANDO AMBAYE ALITESA AFCON NA MALAWI…KAITUPIA SIMBA NENO HILI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply