Klabu ya ma Manchester City wamekubali kumpa mkataba wa paund 500,000 kwa wiki ili kumsajili nyota wa dortmund Erling Haaland. Mkataba ambao utamfanya kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi katika Ligi Kuu ya England.
Jitihada za Manchester City kumsajili Erling Haaland zimepiga hatua kubwa mbele, wakati klabu hiyo ifikiakubaliana na wawakilishi wa mchezaji huyo.Taarifa zinaelewa kuwa kipengele cha kumfanya Haaland kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi kwenye Ligi Kuu ya England imepewa nafasi kubwa ambapo anatarajiwa kulipwa kaisai cha paund 500,000 kwa wiki.
City sasa wanatarajiwa kumuandalia mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21 kwa kitita cha pauni milioni 63 katika klabu ya Borussia Dortmund, na kama mambo yote yataenda kama walivyopanga basi mkataba wa miaka mitano wa nyota huyo kujiunga City utakua umekamilika kuanzia wiki ijayo.
Kulikuwa na matumaini mchezaji huyo kwamba angeongeza mkataba wake kwa mwaka mmoja kuitumikia Dortmund, Lakini City wameendelea kujiimarisha na kujiamini katika mchakato mzima wa kumnasa nyota huyo na sasa wanakaribia kukamilisha usajili wake.
Kocha wa manchester City Pep Guardiola sasa anaonekana kudhamiria kukamilisha uhamisho huu baada ya kushindwa kumsajili Harry Kane msimu uliopita, na licha ya kuwa kileleni mwa Ligi lakini wakati fulani City wamekua wakionekana kukosa mshambuliaji wa kati wa kuaminika.