Habari za michezo

BAADA YA AZIZ KI KUSHINDWA KUONYESHA KIWANGO JUZI….LUNYAMILA AIBUKA NA KUMNYOOSHEA KIDOLE…

admin August 11, 2022 2:42 am


Winga wa zamani wa Yanga, Edibily Lunyamila amekiangalia kikosi cha Yanga na kutamka moto utawaka huku akimwagia sifa kiungo Stephane Aziz Ki kwa kudai anajua boli.

Jumamosi iliyopita, Yanga ilifanya tamasha la Wiki ya Mwananchi ikicheza mechi ya kirafiki ya Kimataifa na mabingwa wa Ligi Kuu Uganda, Vipers na kukubali kichapo cha mabao 2-0, kwenye Uwanja wa Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Lunyamila ambaye amewahi kuichezea Malindi ya Zanzibar, Simba na Taifa Stars ameibuka na kudai Yanga ina wachezaji wazuri kinachohitajika ni kocha Nassreddine Nabi kuwaunganisha ili kupata matokeo mazuri.

“Ili uwe na timu bora ni lazima uwepo muda wa kuzoweana na katika maandalizi ya msimu unaweza kucheza vizuri lakini kwenye ligi usipate matokeo mazuri nadhani kocha wetu Nabi atakuwa ameona makosa na atakuwa anayafanyia kazi,” alisema.

Lunyamila ambaye alikuwa akisifika kwa uwezo wake wa kupiga chenga alisema anaamini Nabi bado ana muda na atafanya marekebisho kabla ya kwenda katika michezo ya kimashindano.

KISA YANGA…ZORAN AJIFUNGIA CHUMBANI KWA MASAA MAWILI….HERSI AUNDA TIMU YA USHINDI KWA YANGA NNJE YA UWANJA… IMEFICHUKAAA….SIMBA DAY CHANZO CHA MENEJA UWANJA WA TAIFA KUTUMBULIWA….ISHU YA JENEZA YAHUSISHWA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply