Wakala wa wachezaji maarufu Dunia Mino Raiola 54β² amefariki Dunia mchana wa leo Jumamosi, Aprili 30, 2022 baada ya kuugua kwa muda mfupi akiwa nyumbani kwake Roma nchini Italia.
Wakala huyo maarufu duniani anawasimamia wachezaji Erling Halaand wa Borrusia Dortmund,Paul Pogba wa Manchester United na Zlatan Ibrahimovich huku akisifika kwa kufanya dili kadhaa za hela ndefu kwa mastaa hao maarufu duniani.
Wakala huyo alizaliwa katika mji wa Nocera Inferiore, Italy mwaka 1967 na alihamia Haarlem nchini Uholanzi akiwa na familia mwaka uliofatia huku akikulia katika maisha ya mpira akiwa kama mchezaji na kisha kama wakala.