Habari za SImba SC
Habari za michezo

WAKATI LEO WAKITANGAZA KUANZA ‘MABALAA’….KIGOGO SIMBA AFUNGUKA USAJILI WAO ULIVYO..

admin June 19, 2023 6:55 pm

HUKU wakiendelea na ukarabati mkubwa wa kikosi chao kupitia usajili, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ amewachimba mkwara mzito wapinzani wao msimu ujao, hususani watani zao wa jadi Yanga kwa kuweka wazi kuwa hawatakuwa wanyonge tena na wanasuka kikosi cha mataji.

Simba imekuwa na ukame wa misimu miwili mfululizo bila taji lolote kubwa, huku wakishuhudia mataji hayo yote yakibebwa na watani Yanga hali ambayo imewafanya mashabiki wengi wa Simba kuingia jazba.

Tayari Simba imetangaza kuachana na mchezaji Augustine Okrah na baadhi ya watendaji wa benchi la ufundi, huku leo Jumatatu wakitarajiwa kuendeleza panga lao kwa ajili ya kupata nafasi ya kushusha mashine mpya.

Akizungumzia usajili na mipango yao kuelekea msimu ujao, Try Again alisema: “Nawahakikishia Wanasimba wote kuwa msimu ujao hatutakuwa wanyonge tena, tutakuwa imara kuliko ilivyokuwa awali.

“Tunajua kwa misimu miwili hatukuwa na furaha hususani katika suala la kushinda mataji, lakini msimu ujao tutakuwa bora kwakuwa tutasajili kikosi imara.”

WAZUNGU WALIOLETWA NA SIMBA BONGO WAANZA NA MZIZE….SILI LAKE LAPELEKWA KIMYA KIMYA.. HUYU HAPA KOCHA LA PASI MILIONI ANAYETAJWA KUTUA YANGA….SOKA LAKE NI ‘SUKARI TUPU’…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply