Home Habari za michezo ALIYEMTUNGUA MANULA…..AANZA KUVIMBA KIBABE…ACHIMBA MKWARA WA KUFA MTU…

ALIYEMTUNGUA MANULA…..AANZA KUVIMBA KIBABE…ACHIMBA MKWARA WA KUFA MTU…


Kiungo wa Coastal Union, Mnigeria Victor Akpan juzi aliifunga Simba bao la kideoni kwa kumtungua kipa Aishi Manula na baada ya hapo alichimba mkwara kwa makipa wengine.

Licha ya chama lake kupoteza nyumbani kwa kupigwa mabao 2-1 na Mnyama Simba lakini bao la Akpan lilikuwa la kusisimua pia la huzuni kwa Simba kutokana na mazingira ya upatikanaji wake.

Wakati Simba ikiongoza kwa bao 1-0 hadi dakila ya 75, dakika ya 76 Akpan akiwa nje ya boksi la 18 la Simba alipokea mpira na kuutuliza kisha kupiga shuti la kuzungusha liilozama moja kwa moja nyavuni na kuisawazishia Coastal kabla ya Meddie Kagere kufunga bao la ushindi kwa Simba dakika ya 90.

Akipiga stori baada ya mechi ile, Akpan alieleza amekuwa akifunga mabao ya vile kwa muda mrefu na kuwatshadharisha makipa wa timu pinzani kuwa makini zaidi.

“Sio mara ya kwanza kufunga vile, nimekuwa nikifunga kila nikipata nafasi hivyo jana ilikuwa muendelezo tu.

Makipa wanahitaji kuwa makini wakiwa langoni vinginevyo nitaendelea kuwafunga,” alisema.

SOMA NA HII  USAJILI WA SIMBA WAITISHA YANGA, ALLY KAMWE AJITETEA