Home Habari za michezo BAADA YA KUONA KIWANGO CHA NGUSHI JUZI..NABI KAINAMISHA KICHWA KISHA AKASEMA HAYA…

BAADA YA KUONA KIWANGO CHA NGUSHI JUZI..NABI KAINAMISHA KICHWA KISHA AKASEMA HAYA…


BAADA ya Yanga kuvuna ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Azam FC, Kocha Mkuu wa timu hiyo, raia wa Tunisia, Nasreddine Nabi, amesema kuwa ndani ya miaka miwili ijayo Chripine Ngushi atakuwa bonge la straika tishio hapa nchini.

Yanga imeendelea kujikita kwenye kilele cha ligi ikiwa na pointi 51, ilizozivuna baada ya kushuka dimbani mara 19, ikiwaacha jumla ya pointi 14 watani wao Simba waliopo nafasi ya pili na pointi 37, walizozivuna baada ya kucheza mechi 17 kabla ya mchezo wa jana dhidi ya Coastal Union.

Baada ya kuwafunga Azam FC, Jumapili hii Yanga inatarajia kucheza na Geita Gold kwenye hatua ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho la Azam Sports, Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Nabi amesema, kuwa kwenye mchezo wao na Azam FC, baada ya kuwaona wamekamia zaidi na kwamba walikuwa wakitumia upande wao wa kushoto ambao alikuwa akicheza Bruce Kangwa, akaamua kumtoa Dickson Ambundo na kumuingiza Ngushi ili ambane ili wapate nafasi ya kushambulia.

“Ngushi ni kati ya mastraika wakubwa sana ninaowaangalia baada ya miaka miwili ijayo, ambapo Tanzania itapata hazina kubwa sana, hivyo nina imani hata uwepo wake ndani ya Yanga, atatusaidia zaidi kwani kama asingepata majeraha baada ya kujiunga nasi tu leo hii angekuwa ameshaonyesha maajabu zaidi,” alisema Nabi.

SOMA NA HII  YANGA WAFUNGUKA SABABU ZA MAKOCHA WAO KUTOWEKA