Home Habari za michezo HUKO UINGEREZA UBINGWA MSIMU HUU NI ZAIDI YA VITA YA UKRAINI NA...

HUKO UINGEREZA UBINGWA MSIMU HUU NI ZAIDI YA VITA YA UKRAINI NA URUSI…MAN CITY AKITELEZA TU…


Msimamo wa Ligi Kuu England unavyosomeka kwa sasa, Manchester City ipo juu kabisa na pointi zao 73 baada ya kushuka uwanjani mara 30.

Bado mechi nane mbele yao na kama wataendelea kutulia kwenye eneo hilo watabeba ubingwa wa msimu huu.

Lakini, nyuma yao wapo Liverpool wenye pointi 72 na wao wamebakiza mechi nane kukamilisha msimu. Hivyo, miamba hiyo ni vuta nikuvute kwenye mbio za ubingwa wa msimu huu, huku Aprili 10 inaweza kuamua nani atakwenda kubeba taji hilo, wakati miamba hiyo itakapochuana yenyewe kwa wenyewe uwanjani Etihad.

Ushindi wa wenyeji Man City utawafanya kutanua pengo la pointi na kufikia nne kileleni, lakini kama Liverpool itaibuka wababe, basi watapanda kileleni na kutengeneza pengo la pointi mbili. Shughuli ni pevu.

Kazi nzito kwa makocha wa miamba hiyo, Pep Guardiola na Jurgen Klopp, ambao wamekuwa wakichuana kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England katika misimu ya karibuni.

Wakati mashabiki wa ligi hiyo wakisubiri kuona ni nani atabeba ubingwa na pengine zile timu zitakazokuwamo ndani ya Top Four, mikikimikiki hiyo imeweka rekodi kibao, ambapo kila timu inayo yake ya kujivunia.

Hizi hapa rekodi za kibabe kabisa zinazomilikiwa na timu kwenye Ligi Kuu England.

-Ubingwa mara nyingi, Manchester United – 13

-Ubingwa mara nyingi mfululizo, Manchester United – 3

-Ubingwa wa tofauti kubwa ya pointi, Manchester City – pointi 19

-Ubingwa wa tofauti ndogo, Manchester City – tofauti ya mabao 8

-Ubingwa wa mapema, Liverpool – mechi 31

-Ubingwa wa pointi nyingi kwa msimu, Manchester City – pointi 100

-Pointi nyingi kwa msimu bila ya kubeba ubingwa, Liverpool – pointi 97

-Timu iliyopata pointi chache kwa msimu, Derby County – pointi 11

-Timu iliyobeba ubingwa na pointi chache kwa msimu, Manchester United – pointi 75

-Timu iliyopata pointi nyingi na bado ikashuka daraja, West Ham United – pointi 42

-Timu iliyopanda daraja na kupata pointi nyingi, Ipswich Town – pointi 66

-Timu iliyopata ushindi mara nyingi kwenye Ligi Kuu England, Manchester United – 692

-Timu iliyopata ushindi mara nyingi nyumbani, Liverpool – mechi 24

SOMA NA HII  BAADA YA KUGUNDUA MBINU ZA WATUNISIA...NABI KAGUNA WEE..KISHA AKASEMA HAYA...

-Timu iliyopata ushindi mara nyingi ugenini, Manchester City – mechi 12

-Timu iliyocheza mechi nyingi bila ya kushinda, Sheffield United – mechi 17

-Timu ya kwanza kuzishinda karibu kila timu ndani ya msimu, Chelsea

-Timu iliyokumbana na vichapo vingi, Everton – 398

-Timu iliyokumbana na vichapo vichache, Arsenal – 0

-Timu iliyocheza mechi nyingi mfululizo bila ya kupoteza, Arsenal – mechi 49

-Timu iliyocheza mechi nyingi mfululizo bila ya kupoteza nyumbani, Chelsea – mechi 86

-Timu iliyocheza mechi nyingi mfululizo ugenini bila ya kupoteza, Manchester United – mechi 29

-Timu iliyokumbana na vichapo vingi mfululizo, Sunderland – mechi 20

-Timu iliyopata sare nyingi kwenye Ligi Kuu, Everton – mechi 315

-Timu iliyocheza mechi nyingi mfululizo bila ya kupata sare, Tottenham Hotspur – mechi 32

-Timu iliyofunga mabao mengi kwa msimu mmoja, Manchester City – mabao 106

-Timu iliyofungwa mabao machache ndani ya msimu, Chelsea – mabao 15

-Timu iliyomaliza juu licha ya kuwa na hasi kwenye tofauti ya mabao, Norwich City, -4

-Timu iliyomaliza chini licha ya kuwa na chanya kwenye tofauti ya mabao, Manchester City +1

-Timu iliyofunga bao katika kila mechi ya msimu, Arsenal

-Timu iliyofunga mabao katika mechi nyingi mfululizo, Arsenal – mechi 55

-Timu iliyoonyeshwa kadi nyingi za njano, Chelsea – kadi 1,739

-Timu iliyoonyeshwa kadi nyingi nyekundu, Arsenal – kadi 100

-Timu iliyoonyeshwa kadi nyingi za njano ndani ya msimu mmoja, Sunderland – kadi 94

-Timu iliyoonyeshwa kadi chache za njano ndani ya msimu mmoja, Coventry City – kadi 12

-Timu iliyoonyeshwa kadi nyingi za njano katika mechi moja, Tottenham Hotspur – kadi 9

-Timu iliyopewa penalti nyingi ndani ya msimu mmoja, Manchester United – 14

-Timu iliyoruhusu penalti nyingi ndani ya msimu mmoja, Hull City – 13

-Timu iliyoshinda mara nyingi Kiatu cha Dhahabu, Arsenal – 6

-Timu iliyotoa washindi wengi wa Kiatu cha Dhahabu, Manchester City – 6

-Timu iliyoweka rekodi ya mechi yake kutazamwa na mashabiki wengi, Tottenham Hotspur – mashabiki 83,222.