Home CAF BAADA YA KUONA WAMEPANGWA NA SIMBA…WASAUZI WAMESHIKA KICHWA HUKO…BOSSI WAO KAJIFARIJI NA...

BAADA YA KUONA WAMEPANGWA NA SIMBA…WASAUZI WAMESHIKA KICHWA HUKO…BOSSI WAO KAJIFARIJI NA HILI…


Afisa Mtendaji Mkuu ‘CEO’ wa Orlando Pirates Floyd Mbele amesema wameipokea kwa mikono miwili Droo ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Hafla ya kuchezesha Droo ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho ilifanyika juzi Jumanne (April 05), mjini Cairo-Misri na klabu hiyo ya Afrika Kusini ilipangwa kukutana na Simba SC ya Tanzania.

Mbele amesema wanaifahamu vizuri Simba SC na wanatarajia mchezo wenye ushindani kutoka kwa mabingwa hao wa Tanzania Bara, ambao wananolewa na Kocha Franco Pablo Martin kutoka Hispania.

Amesema Orlando Pirates ipo tayari kwa Robo Fainali ambapo mchezo wa mkondo wa kwanza utachezwa Dar es salaam-Tanzania, Uwanja wa Benjamin Mkapa kati ya April 15-17, huku mchezo wa Mkondo wa pili ukitarajiwa kupigwa Afrika Kusini kati ya April 22-24.

Kiongozi huyo pia amemzungumzia Mshambuliaji hatari wa kikosi chao Gabadinho kwa kusema yupo vizuri na ana matumaini makubwa ya kucheza michezo yaote, nyumbani na ugenini.

“Tunawajua Simba vizuri,tunajua mpaka kocha wao mpya kutoka Hispania na mpira wanaocheza wamekuepo kwenye mashindano ya CAF kila mara Ila tumejipanga vyema, Gabadinho Yuko Sawa na hakuna tatizo hata mwishoni mwa juma lililopita alicheza dhidi ya Al Itihad.” Amesema Mbele.

Simba SC ilitinga Robo Fainali kwa kishindo Jumapili (April 03), kwa kuifunga USGN ya Niger mabao 4-0 Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Ushindi huo uliifanya Simba SC kumaliza nafasi ya pili katika msimamo wa Kundi D kwa kufikisha alama 10 sawa na RS Berkane ya Morocco, ikizidiwa mabao ya kufunga na kufungwa.

SOMA NA HII  KISA SAKATA LA KISINDA NA TFF....LOMALISA ATEMWA USAJILI WA YANGA...ISHU NZIMA IMEKAA NAMNA HII...