Home Habari za michezo SALEHE JEMBE – NTIBAZONKIZA NI KAMA MVINYO…ANAZIDI KUWA MTAMU….

SALEHE JEMBE – NTIBAZONKIZA NI KAMA MVINYO…ANAZIDI KUWA MTAMU….


UBORA wa Saido Ntibazonkiza umeendelea kuwa juu tangu sakata lake la utovu wa nidhamu na Klabu ya Yanga kumalizika.

Kwa mujibu wa Salehe Ally ‘Jembe’ Mchambuzi wa kipindi cha Krosi Dongo kinachorushwa na Global TV na Global Radio anadai Saido ni kama mvinyo kadri anavyozidi kuzeeka ndivyo anavyozidi kuwa mtamu katika soka

Kwa asilimia kubwa mchezo wa jana uliamuliwa na ubora wa Saido maana yeye ndiye mchezaji aliyechezewa faulo nyingi sana lakini pia utimamu wake wa mwili ulikuwa wa hali ya juu hadi kufanikiwa kumaliza dakika zote 90 licha ya kwamba ametoka kuoa hivijuzi tu.

Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa  moja dhidi ya Klabu ya Azam huku mfungaji wao kinara wa mabao Fiston Mayele akifanikiwa kufunga bao la pili na kufikisha idadi ya mabao 11 akiwa kinara katika msimamo wa Wafungaji Bora wa Ligi Kuu ya NBC mpaka sasa.

SOMA NA HII  BEKI HUYU AKITUA TU PALE YANGA...BAKARI MWAMNYETO HUENDA AKACHEZEA YANGA B...