Home Habari za michezo SAKATA LA FEI TOTO NA YANGA….KWA MARA YA KWANZA SENZO AFUNGUKA MCHEZO...

SAKATA LA FEI TOTO NA YANGA….KWA MARA YA KWANZA SENZO AFUNGUKA MCHEZO ULIVYO…AITAJA CAS…

Habari za Yanga

Senzo Mbatta aliyekuwa CEO wa Simba SC na Yanga SC kwa nyakati tofauti, amesema kesi ya Feisal Salum kama ataenda CAS itakuwa ngumu kwake kwa babu kuna vitu vingi amekosea.

Senzo amesema; “Maombi ya Feisal Kuvunja mkataba na yeye kwenda kuilipa Yanga kabla ya kutuma maombi ya kuvunja huo mkataba na kuanisha sababu za kutaka kuvunja mkataba.

“Muda wa kuvunja mkataba haukuwa sahihi huwezi kufanya jambo kama hili katikati ya msimu bila sababu maalumu maana sheria zipo wazi zinasema lazima uainishe vifungu vilivyokiukwa kwenye mkataba wako ndio uvunje mkataba.

“Timu iliyomtaka ilipaswa lazima iandike barua Yanga kabla ya kulipa release clause ya kiasi kilichoanishwa.

“Iwapo imetokea bahati imewezekana Feisal Salum anavunja mkataba , Sheria za FIFA zimesema itawezekana siku 15 kabla ya mwisho wa msimu kama kutakuwa na mazingira magumu kwake [Difficult Case].”

Senzo amemaliza kwa kusema Kwa maana hiyo FEITOTO ana makosa mengi amefanya, ila FIFA Hawawezi kumfungia ila watamuambia arudi klabuni acheze.

SOMA NA HII  TANZANIA YAOMBA KUANDAA AFCON 2027...SERIKALI YABARIKI...VIWANJA VYA SIMBA NA YANGA KUTUMIKA...