Home Uncategorized ROLLERS: YANGA SIO WA MCHEZOMCHEZO, TUTAPAMBANA NAO KIBISHI NYUMBANI

ROLLERS: YANGA SIO WA MCHEZOMCHEZO, TUTAPAMBANA NAO KIBISHI NYUMBANI


THOMAS Truch, Kocha Mkuu wa Township Rollers amesema kuwa wamepambana na kikosi chenye ushindani jambo lililofanya wapate sare licha ya kutangulia kufunga.

Rollers jana ilikubali kupata sare ya kufungana na kikosi cha Yanga bao 1-1 uwanja wa Taifa licha ya kuanza kupachika bao la kuongoza mapema dakika ya 7.

“Yanga ni timu bora ndio maana wamepata matokeo chanya, kwa kuwa wao walikuwa kwao nasi ni wakati wetu kujiaanda kupata matokeo chanya tukiwa nyumbani.

“Walikuwa na nafasi ya kushinda kama ilivyokuwa kwetu mwisho wa siku matokeo ndio kama ilivyo nasi tunaamini mchezo wa nyumbani utakuwa mgumu,” amesema.

Rollers msimu wa mwaka 2018 ililazimisha sare ya bila kufungana kwenye mchezo wa marudio uliochezwa nchini Botswana, mchezo wa kwanza walishinda kwa mabao 2-1 uwanja wa Taifa hivyo kazi bado ni ngumu kwa timu zote mbili.

Yanga inatakiwa kushinda kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa kati ya Agosti 23-25 nchini Botswana.

SOMA NA HII  MZUNGUKO WA 10 KUNA MAMBO YA KUJIFUNZA, LIGI DARAJA LA KWANZA ISIPEWE KISOGO