Home Geita Gold FC KUMBE ILIBAKI HIVII TUUH MPOLE ASAINI MSIMBAZI….MWENYEWE AFUNGUKA DILI LILIVYOBUMA WAKAHAMIA KWA...

KUMBE ILIBAKI HIVII TUUH MPOLE ASAINI MSIMBAZI….MWENYEWE AFUNGUKA DILI LILIVYOBUMA WAKAHAMIA KWA ‘MZUNGU’….


Kinara wa upachikaji wa mabao msimu uliopita kwenye Ligi Kuu Bara, Mshambuliaji wa Geita Gold George Mpole amefunguka sababu za kushindwa kusaini Simba ni suala la maslahi tu.

Mpole ambaye tayari ameongeza mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia Geita Gold amesema ni kweli alipokea ofa kutoka Simba lakini Geita walikidhi maslahi yake ndio maana hakuona umuhimu wa kuondoka klabuni hapo.

“Nilikuwa na ofa nyingi kutoka timu za ndani na nje ya Tanzania ila nimeamua kubaki kwa sababu wameweza kunitimizia mahitaji yangu.” amesema Mpole na kuongeza;

“Kuhusu kuzungumzwa kwamba nimechelewa kusaini mkataba na Geita Gold sio kweli, ni timu ambayo nashirikiana nayo kwenye kila kitu na suala la ofa zangu za nje taarifa hizo wanazo,” amesema.

Nyota huyo alikuwa sehemu ya kikosi cha Geita katika mchezo wa kwanza wa ufunguzi Ligi Kuu Bara wakati timu yake ilipofungwa mabao 3-0 dhidi ya Simba jana kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

SOMA NA HII  WAZIRI "MWANA FA:- AWAFUNGA MDOMO TFF...NDONDO CUP 2023 ITAFANYIKA