Home Habar za Usajili Simba MAPYA YAIBUKA SAKATA LA MANZOKI KUTUA MSIMBAZI…VIPERS NA WAKALA WAKE WAIVURUGA SIMBA…

MAPYA YAIBUKA SAKATA LA MANZOKI KUTUA MSIMBAZI…VIPERS NA WAKALA WAKE WAIVURUGA SIMBA…


Wakati zikisaliwa takribani siku 13 kabla ya usajili wa dirisha kubwa kufungwa hapa nchini, uongozi wa Simba, umetangaza kuachana mazima na mshambuliaji wa Vipers FC ya Uganda, César Lobi Manzoki.

Hiyo ni katika kuelekea kufungwa kwa usajili Agosti 31, mwaka huu baada ya kufunguliwa Julai Mosi.

Awali Simba ilielezwa kumalizana na mshambuliaji huyo aliyetwaa Tuzo ya Ufungaji na Mchezaji Bora katika Ligi Kuu ya Uganda msimu uliopita kwa ajili ya kukiongezea nguvu kikosi chao.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema baada ya kumtambulisha Mserbia, Dejan Georgijevic, hakuna mchezaji mwingine watakayemsajili kipindi hiki.

Aliongeza kuwa, kutokana na utata uliopo katika ukomo wa mkataba wa Manzoki na timu yake ambapo mwenyewe anasema unaisha Oktoba mwaka huu, huku Vipers ikisema utaisha 2024, ndiyo sababu ya kuachana naye.

“Kama uongozi tumechukua uamuzi wa kuachana na Manzoki, labda hadi katika dirisha dogo au msimu mwingine, hivyo Dejan ndiye amefunga usajili wetu.

“Manzoki mkataba wake haupo wazi kwa pande zote mbili, yeye mwenyewe anasema ana mkataba wa miezi miwili, lakini timu yake inasema ana mkataba hadi 2024.

“Hiyo imesababisha mazungumzo kuwa magumu, hivyo tumesitisha mipango hiyo ya kumsajili Manzoki kwa hivi sasa, labda yatokee mabadiliko mengine kabla ya usajili kufungwa,” alisema Ally.

SOMA NA HII  KUELEKEA SIMBA DAY....KIBADENI AIBUKA NA HILI JIPYA...ATOA KILIO CHA WACHEZAJI WAKONGWE...MGOSI AKAZIA...

1 COMMENT

  1. What’s Going down i’m new to this, I stumbled upon this I’ve found It absolutely helpful and it has helped me out loads. I’m hoping to contribute & help different users like its helped me. Great job.