Home Habari za michezo KISA SARE MBILI MFULULIZO….KLOPP AINGIA KWENYE KASUMBA ZA KURONGWA…ADAI WACHEZAJI WAKE...

KISA SARE MBILI MFULULIZO….KLOPP AINGIA KWENYE KASUMBA ZA KURONGWA…ADAI WACHEZAJI WAKE WAMECHEZEWA…


KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kwa utani kwamba wachezaji wake wanarogwa walipopata sare ya 1-1 dhidi ya Crystal Palace katika mchezo wa Ligi Kuu England uliofanyika juzi Jumatatu.

Liverpool imekuwa ikiandamwa na majeruhi wengi msimu huu ambapo ilikosa mastaa wake kadhaa kwenye uteuzi wa kikosi chao kilichomenyana na Crystal Palace huko Anfield juzi.

Joel Matip alipata maumivu ya misuli ya korodani mazoezini, wakati Roberto Firmino naye alikosa mechi hiyo kwa tahadhali ya kumfanya aumie zaidi.

Diogo Jota, Thiago Alcantara, Ibrahima Konate, Caoimhin Kelleher, Alex Oxlade-Chamberlain, Curtis Jones na Calvin Ramsay nao wapo kwenye chumba cha wagongwa kwenye kikosi hicho cha Klopp, wakati Kostas Tsimikas, Jordan Henderson na Naby Keita hawakuwa fiti kuanza mechi, bali walilazimika kuwapo tu benchi.

Mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya bao 1-1 na hivyo kuwafanya Liverpool kutoshinda mechi yoyote kwenye Ligi Kuu England msimu huu na jambo hilo linamfanya kocha Klopp kudai majeruhi ya wachezaji wake yanatokana na kurogwa.

“Hii wiki hatari sana. Nimeshuhudia wiki nyingi zaidi hii, lakini naweza kusema kuna mchawi kwenye hili jengo. Ona, kila siku kuna mtu anashindwa kufanya mazoezi kwa sababu zisizoeleweka kabisa,” alisema Klopp.

Katika mchezo huo, Liverpool ilimshuhudia straika wake mpya iliyemsajili kwa pesa nyingi, Darwin Nunez akitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumpiga kichwa Joachim Andersen.

Jambo hilo litamfanya Nunez kukosa mechi dhidi ya Manchester United, Bournemouth na Newcastle United na anatarajia kurudi uwanjani kwenye kipute cha Merseyside derby kitakachopigwa nyumbani kwa Everton, Goodison Park, Septemba 3.

SOMA NA HII  MSHAMBULIAJI LIGI KUU AWEKA WAZI...WANASUBIRIA MIUJIZA ITENDEKE...AMEZUNGUMZA HAYA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here