Home Habari za michezo PAMOJA NA KUKOSA MAGOLI JUZI…KAGERE APEWA HESABU YA MAGOLI 15 KWA MSIMU...

PAMOJA NA KUKOSA MAGOLI JUZI…KAGERE APEWA HESABU YA MAGOLI 15 KWA MSIMU HUU….HANS PLUIJM ABAKI KUCHEKA TU…


Kocha wa Singida Big Stars, Hans van der Pluijm anaamini mshambuliaji wake, Meddie Kagere anaweza kumaliza msimu akiwa na zaidi ya mabao 15.

Pluijm anaamini raia huyo wa Rwanda aliyezaliwa Uganda, anaweza kuendelea kucheka na nyavu Ligi Kuu Bara kama ilivyokuwa Simba ambako ameondoka akiwa mmoja wa wachezaji hatari wa kigeni ambao wameifanyia makubwa klabu hiyo.

β€œNamtazama kama mmoja wa wachezaji muhimu kwenye kikosi changu. Ni mzoefu na ningependa kuona uzoefu wake ukiisaidia timu, sina shaka na ubora wake kwa sababu tayari ameshathibitisha hilo na huu utakuwa ni muendelezo tu,” alisema.

Huu ni msimu wa tano kwa Kagere kucheza Ligi Kuu ambapo wa kwanza alimaliza na mabao 23 (2018/19), uliofuatia akatupia 22 (2019/20), mwingine alikuwa nayo 13 (2020/21) na uliopita alitupia mabao saba.

Katika kikosi cha Singida Big Stars, Meddie amekutana na Amiss Tambwe ambaye naye kwa wakati wake alifanya makubwa Ligi Kuu Bara.

Takwimu zinaonyesha kuwa Tambwe ndani ya msimu wake wa kwanza 2013/14 alikuwa na mabao 19, alipohamia Yanga 2014/15 (mabao 14), 2015/16 (mabao 21), 2016/17 (mabao 11) na 2018/19 (mabao nane).

Washambuliaji hao ni miongoni mwa silaha ambazo Pluijm anazitegemea msimu huu kwenye safu yake ya ushambuliaji.

SOMA NA HII  KOSA LA SIMBA KUSHINDWA KUTAMBA KIGALI....... HILI HAPA