Home Habari za michezo KOSA LA SIMBA KUSHINDWA KUTAMBA KIGALI……. HILI HAPA

KOSA LA SIMBA KUSHINDWA KUTAMBA KIGALI……. HILI HAPA

Habari za Simba SC

Meneja wa Habari na Mawasiliano, Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema baada ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya Power Dynamos, kikosi kinarejea nchini kujipanga na mchezo wa marudiano ambao utapigwa Oktoba mosi nchini Tanzania.

Ahmed amesema walitarajia mchezo huo kuwa na ushindani kwa kuwa Power Dynamos sio timu nyepesi, wakiwa mabingwa wa ligi kuu ya Zambia.

“Tulitarajia mchezo hautakuwa mwepesi, mchezo huu umetupa kipimo sahihi cha mechi ya ligi ya mabingwa. Hatukuwa vizuri sana kwenye kipindi cha kwanza, lakini unaona tulirejea tukiwa imara zaidi kwenye kipindi cha pili na pengine tulistahili kushinda mabao mengi.

“Sare hii waliyoipata sio kwa sababu ya ubora wao lakini pia imechangiwa na makosa katika upande wetu. Tumepoteza nafasi nyingi za wazi kama Baleke na Saido wanefunga nafasi walizopata pengine leo tungekuwa tukizungumza mengine.

“Lakini pia bao la pili walilotufunga lilitokana na makosa ya mlinda lango wetu, hivyo kwa ujumla wake tumeyapokea matokeo haya na tunakwenda kujipanga kwa ajili ya mchezo wa marudiano nyumbani.

“Tutakwenda kumaliza kazi jijini Dar es salaam, Simba hii sio ya kutolewa na Power Dynamos katika mashindano haya. Tumejua wapi tumekosea katika mchezo wa kwanza hivyo tutakwenda kujisahihisha nyumbani ili tufuzu hatua ya makundi,” alisema Ahmed.

Kikosi cha Simba kinatarajiwa kurejea Tanzania leo kujiandaa na mchezo unaofuata kwenye ligi kuu dhidi ya Coastal Union utakaopigwa Ijumaa ijayo katika uwanja wa Uhuru.

SOMA NA HII  PAMOJA NA UWEPO WA MBOMBO NA MASTAA WENGINE ....AZAM FC KUONGEZA WATATU DIRISHA DOGO...