Home Habari za michezo GAMONDI BADO AWATAMANI AL MAREIKH…….ATOA KAULI HII

GAMONDI BADO AWATAMANI AL MAREIKH…….ATOA KAULI HII

Habari za Yanga SC

Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi licha ya kuwapongeza wachezaji wake amesema walistahili ushindi mkubwa zaidi ya huo dhidi ya wapinzani wao.

Gamondi alisema bado hawajamalizana na Al Merrikh na amewataka wachezaji kusahau haraka matokeo hayo na kuanza kufikiria mechi ijayo ya Ligi Kuu ikiialika Namungo keshokutwa Jumatano, kisha kurudia mchezo wa CAF.

“Tulikuwa na dakika 90 nzuri, nawapongeza sana wachezaji wangu, licha ya ugumu wa mchezo hasa kipindi cha kwanza, ila walirudi kipindi cha pili na akili kubwa ya kutafuta ushindi na tukafanikiwa, tunawaheshimu wapinzani wetu lakini nadhani tulistahili ushindi mkubwa zaidi ya huu kulingana na jinsi tulivyotengeneza nafasi za wazi,”

“Mechi hii ya kwanza imekwisha, sasa tunatakiwa kuhamisha akili kwenye mechi ya ligi na baada ya hapo tutamalizana na wapinzani wetu hao wa CAF, nataka nikwambie bado hatujashinda, ushindi mzuri unatakiwa kuwa mechi hii ya pili, hata wao wanaweza kutufunga kwetu kama hatutakuwa makini.”

Kocha huyo anaisaka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza tangu mwaka 1998 kuivusha Yanga kuingia makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, pia kuandika historia nyingine ya kuing’oa timu ya Sudan kwenye mechi za CAF tangu ilipoanza kushiriki michuano hiyo mwaka 1969.

SOMA NA HII  BOCCO APITA NJIA ZA KINA AY NA FA KIBABE SANA