Home Habari za michezo BAADA YA KUTOA GUNDU JUZI…..MUGALU KAANZA NGEBE…AFUNGUKA ALIYOYAPITIA…ADAI AMEPONA…

BAADA YA KUTOA GUNDU JUZI…..MUGALU KAANZA NGEBE…AFUNGUKA ALIYOYAPITIA…ADAI AMEPONA…


MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu amesema kuwa mabao ambayo amefunga katika mchezo uliopita wa Kombe la Shirikisho dhidi ya USGM ya Niger yamemuongezea hali ya kupambana zaidi jambo ambalo anaamini litamsaidia kuweza kufunga mabao ya kutosha katika michezo ijayo.

Mugalu ambaye amekuwa na msimu mbaya kutokana na majeraha aliyokuwa akiyapata mara kwa mara, katika mchezo huo uliopigwa Jumapili alifanikiwa kufunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 4-0 walioupata Simba na kwenda hatua ya robo fainali.

Mugalu alisema kuwa mabao hayo mawili aliyoyafunga yatamuongezea hamasa ya kutaka kufanya vizuri katika michezo ijayo ambayo atashiriki huku akiweka wazi kufurahia maisha ndani ya timu hiyo.

“Nimefurahi sana kuona nimefunga mabao mawili katika mchezo uliopita, hakuna ambaye hafahamu nini kilitokea huko nyuma juu yangu ila nafurahi kwa sasa kuona nimepona na nimeanza vizuri kwa kufunga.

“Ambacho kipo mbele yangu kwa sasa ni kuona ni namna gani naendelea kuisaidia Simba kufanya vyema kwa kufunga mabao mengi zaidi hivyo nitaendelea kupambana kuhakikisha nafanya hivyo,” alisema Mugalu.

SOMA NA HII  ALICHOKISEMA ALLY MAYAI KUHUSU NANI BORA KATI YA PABLO NA NABI...AWATAJA FEI TOTO NA MORRISON...