Home Habari za michezo BAADA YA KUTUA TZ….KAPOMBE AWAWASHIA MOTO YANGA….”MAONGEZI HAYATAKIWI….TUKUTANE April 30…”

BAADA YA KUTUA TZ….KAPOMBE AWAWASHIA MOTO YANGA….”MAONGEZI HAYATAKIWI….TUKUTANE April 30…”


Mlinzi wa klabu ya Simba Shomari Kapombe amewatoa hofu wapenzi na mashabiki wa klabu hiyo kuelekea mchezo wao wa Kariakoo Derby dhidi ya Yanga mnamo April 30 kwenye dimba la Benjamin Mkapa majira ya saa kumi na moja kamili jioni kuwa wanarejea kwa kishindo kwenye ligi.

Mlinzi huyo wa kulia wa Simba amesema licha ya kutolewa kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya timu ya Orlando Pirates “the Bucanees” ya Afrika Kusini kwenye hatua ya robo fainali bado wanatambua umuhimu wa mchezo dhidi ya Yanga na kuwaahidi kufanya vizuri kwenye mchezo huo.

“Sisi tumerudi na tunaenda kufanya maandalizi kwa ajili ya mchezo huo kwa hiyo naimani maongezi mengi hayatakiwi zaidi ya kwenda kufanya maandalizi ya mchezo huo na kuwa mzuri zaidi upande wetu “amesema Kapombe

Simba na Yanga zitakutana kwenye dimba la Benjamin Mkapa kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara huku Yanga akiwa kileleni mwa msimamo wa ligi akiwa na alama 54 ilhali Simba akiwa na alama 41 sambamba na kuzidiwa mchezo mmoja na Yanga huku kwenye michezo miwili waliyokutana ya msimu huu Yanga alipata ushindi kwenye mchezo wa ngao ya jamii huku mchezo wa ligi wa mkondo wa kwanza wakitoka sare.

SOMA NA HII  SIMBA KUWAFUATA TZ PRISON KWA KASI YA 6G...