Home Habari za michezo BAADA YA PABLO KUAMUA KUMWEKA KANDO KIKOSINI……DILUNGA AAMUA KUMTIMKIA AFRIKA KUSINI…

BAADA YA PABLO KUAMUA KUMWEKA KANDO KIKOSINI……DILUNGA AAMUA KUMTIMKIA AFRIKA KUSINI…


Kiungo wa Klabu ya soka ya Simba ,Hassan Dilunga ameondoka nchini kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya kupata matibabu ya majeraha yanayomkabili kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika Klabu ya Simba, imeeleza kuwa nyota huyo ambaye aliwahi kuitumikia Yanga, ameondoka leo nchini akielekea Afrika Kusini.

Dilunga maarufu ”HD” amekuwa nje ya dimba kuwa muda mrefu akiuguza jeraha ambalo limemfanya asiitumikie Simba kwa muda mrefu.

Nyota huyo alijiunga na Simba mwaka 2018 na kuwa sehemu ya mafanikio ya mataji mbalimbali waliyoyatwaa Simba kwa misimu miwili mfululizo.

Itakumbukwa kuwa hivi karibuni kocha Mkuu wa Simba Pablo alimtoa kwenye mipango yake yote kiungo huyo kwa msimu huu wa mashindano kutokana na kupatwa na jeraha hilo kubwa.

SOMA NA HII  SAKATA LA KIFUNGO CHA MANARA...WANASHERIA WA MAHAKAMA WAIBUKA NA HOJA HIZI NONDO...WADAI INAWEZEKANA VIPI...