Home Habari za michezo BREAKING NEWS….SIMBA KUKIPIGA NA ORLANDO PIRATES YA AFRIKA KUSINI ROBO FAINAL SHIRIKISHO...

BREAKING NEWS….SIMBA KUKIPIGA NA ORLANDO PIRATES YA AFRIKA KUSINI ROBO FAINAL SHIRIKISHO AFRIKA…


Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kimataifa Simba SC, Watapambana na Orlando Pirates ya Afrika ya Kusini mchezo wa Robo Fainali Kombe la Shirikisho Afrika.

Ratiba hiyo ni kwa mujibu wa Droo iliyochezeshwa leo April 5 nchini Misri na Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika, CAF.

Simba wamefuzu hatua baada ya kukamata nafasi ya pili akitokea kundi D, sambamba na RS Berkane aliemaliza kinara.

Mechi za Robo fainali zitachezwa kati ya Aprili 15 mpaka 17 na mechi za Mkondo wa pili zitapigwa Aprili 22 mpaka 24.

Orlando Pirates ni timu ya zamani ya Bernard Morrisoni, ambapo alikuwa anacheza huko kabla ya kusajiliwa na Yanga kisha Simba.


SOMA NA HII  GAMONDI ATAMBA AWEKA MAMBO HADHARANI