Home Habari za michezo KISA SIMBA…INJINIA HERSI AIONDOA YANGA KIMATAIFA…WADAI LENGO LAO NI NDANI KWANZA…

KISA SIMBA…INJINIA HERSI AIONDOA YANGA KIMATAIFA…WADAI LENGO LAO NI NDANI KWANZA…


Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Hersi Said amesema kwamba licha ya baadhi ya watu kuanza kuipigia hesabu michuano ya kimataifa msimu ujao, hilo kwasasa sio kipaumbele chao bali wanachokiwaza ni kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara ambao pia unawaniwa na Simba SC wakiwa ni mabingwa watetezi.

Hersi ambaye ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM amesema kuwa mara zote yeye huwa anafikiria kilicho mbele yake na anachofahamu ni kwamba wana Yanga wote wana kiu ya kutwaa Ubingwa wa NBC.

”Kama nilivyosema awali ni kuwa tulikuwa tunaijenga klabu yetu ili tufanikiwe kwenye mashindano ya ndani, ukishalifanikisha hilo ndipo tutaweza kupambana kwenye michuano ya kimataifa na hilo lipo katika mipango yetu” Hersi Said Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM.

Katika hatua nyingine Hersi amesema wanajiandaa kwa ajil ya kuwakabili watani zao wa jadi Simba katika mchezo wa tarehe 30 ambao utatoa taswira pana juu ya safari yao ya ubingwa msimu huu.

SOMA NA HII  UNAAMBIWA HIVI NDIVYO YANGA ULIVYOJIANDAA KUISHI BILA YA WACHEZAJI HAWA