Home Habari za michezo STARS KULAMBA BILIONI 17 ZA AFCON….ISHU NZIMA IKO HIVI….

STARS KULAMBA BILIONI 17 ZA AFCON….ISHU NZIMA IKO HIVI….

Taifa Stars

Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ itazawadiwa Dola milioni 7 ambazo sawa na Sh bilioni 17.56 endapo itachukua ubingwa wa Michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) 2023 nchini Ivory Coast.

Kiasi hicho cha fedha ni kufuatia ongezeko la asilimia 40 lililotangazwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Washindi wa pili watapata $4m, huku kila mmoja kati ya wawili waliofuzu nusu fainali atazawadiwa $2.5m, kwa mujibu wa taarifa ya CAF leo.

Kila mmoja wa washindi wanne wa robo fainali atalipwa $1.3m katika muundo mpya wa malipo kwa tukio kubwa zaidi la mchezo mmoja barani Afrika.

Rais wa CAF, Dk Patrice Motsepe alisema: “CAF imepata maendeleo makubwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita katika kuongeza pesa za AFCON na mashindano yake mengine yote makubwa.

“Tumeongeza fedha za zawadi za mshindi wa AFCON hadi Dola 7,000,000 ikiwa ni ongezeko la asilimia 40 kutoka fedha za awali za AFCON.

“Nina imani kuwa sehemu ya fedha za zawadi zitachangia katika kuendeleza soka na pia kuwanufaisha wadau wote wa soka, na pia kusaidia Vyama vyetu vya Wanachama katika tawala zao.”

Michuano hiyo itafanyika kuanzia Januari 13 hadi Februari 11 nchini Ivory Coast. Taifa Stars imepangwa kundi F na timu za DR Congo, Morocco na Zambia.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA CHAMA KUTUA ...SIMBA WAAMUA KUANIKA KILA KITU WAZI..BARBARA ATAJWA KUINJINIA...