Home Habari za michezo KUELEKEA KARIAKOO DABI…MWAMUZI KAYOKO KUKABIDHIWA RUNGU LA UAMUZI…ANABAHATI NA YANGA…

KUELEKEA KARIAKOO DABI…MWAMUZI KAYOKO KUKABIDHIWA RUNGU LA UAMUZI…ANABAHATI NA YANGA…


SIKU chache baada ya Gazeti la  Mwanaspoti kufichua juu ya waamuzi waliokuwa wakipewa nafasi kubwa ya kuchezesha mchezo wa Kariakoo Derby, huku kikao kizito kikifanyika, ukweli umebainika kwamba mwamuzi Ramadhan Kayoko amepewa kazi hiyo.

Hadi Kamati ya Waamuzi inakaa kikao majina matano ndiyo yalikuwa yakipigiwa kura lakini mwisho wa yote, Kayoka ameonekana kupata asilimia kubwa na kupewa jukumu hilo la kumaliza ubishi kwa wababe hao wa soka nchini.

Awali, katika majina hayo matano, lilikuwa jina la Sasii na Abdalla Mwinyimkuu yaliyopewa nafasi kubwa, huku wengine wakiwa ni Hance Mabena, Emmanuel Mwandembwa na Abel William.

Hata hivyo, kikao kilichomalizika katikati ya usiku mwingi kikihusisha Kamati ya Waamuzi, kililiongeza jina la Kayoko na mwishoni mwamuzi huyo kijana akafanikiwa kuwabwaga wenzake.

Taarifa ambazo zimeripotiwa na Gazeti la MwanaSpoti, ni kwamba Kayoko atasimama katikati huku akisaidiwa na Frank Komba (Dar es Salaam), Mohamed Mkono (Tanga), wakati Elly Sasii (Dar es Salaam) atakuwa mwamuzi wa mezani.

Rekodi zinaonyesha kuwa, Kayoko mara ya mwisho kuchezesha dabi ilikuwa Septemba 25, 2021 kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii, akisaidiwa na Frank Komba, Soudy Lila na Sasii aliyekuwa mezani, Yanga ilishinda bao 1-0 likifungwa na Fiston Mayele dakika ya 12.

Mwamuzi huyo ndiye aliyechezesha pia ile dabi ya nusu fainali Kombe la ASFC 2019-2020 iliyopigwa Julai 12, 2020 mchezo ambao waamuzi sita walihusika ni; Komba, Mpanga, Nadeem Aloyce, Abdalah Mwinyimkuu na Abubakari Mturo, na Yanga ikapoteza kwa mabao 4-1.

Pia alichezesha katika mchezo wa kilele cha Siku ya Mwananchi Agosti 29, mwaka jana wakati Yanga ikipoteza kwa mabao 2-1 mbele ya Zanaco kwenye Uwanja wa Mkapa.

Kayoko ambaye alikuwa mwamuzi bora wa msimu wa mwaka 2019/20 hajahusika sana kuchezesha kwenye ratiba ya Ligi Kuu msimu huu hasa michezo inayowahusu wababe hao wa soka la Bongo.

Katika michezo 19 iliyocheza Simba, Kayoko hajachezesha mchezo hata mmoja wakati Yanga iliyocheza michezo 20, Kayoko amechezesha mchezo mmoja wakati ikiichapa bao 1-0 Geita Gold Machi 6, mwaka huu.

SOMA NA HII  KOCHA MPYA SIMBA AANZA NA MKWARA

Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza waamuzi wasaidizi alikuwapo Fedrinand Chacha, Makame Mdogo wakati mwamuzi wa akiba akiwa Wilson Masea.

Katika dabi iliyopita Desemba 11 timu hizo zilipotoka suluhu, mwamuzi wa kati alikuwa, Sasii akisaidiwa na Mpanga, Hamdani Saidi pamoja na Ahmada Simba.

Hili ni pambano la 108 kwa timu hizo katika ligi ya Bara tangu mwaka 1965, lakini ni la 12 kupigwa ndani ya Aprili tangu mwaka 1982.