Home Habari za michezo KUHUSU ISHU YA MABADILIKO YA RATIBA MECHI YA YANGA vs SIMBA…BODI YA...

KUHUSU ISHU YA MABADILIKO YA RATIBA MECHI YA YANGA vs SIMBA…BODI YA LIGI WAJA NA KAULI HII….


Bodi ya Ligi Kuu ya NBC imethibitisha kuwa hadi sasa haijapokea maombi yoyote ya kusogezwa mbele kwa mchezo wa Dabi ya Kariakoo kati ya Simba na Yanga ambao umepangwa kuchezwa April 30,2022.

Akizungumza na East Africa Radio kwenye kipindi cha Michezo cha Kipenga kinachoruka kila siku kuanzia saa 2 hadi saa 3 usiku, Afisa Habari wa TPLB, Karim Boimanda amesema mechi kati ya Simba na Yanga itachezwa katika tarehe na siku ilyopangwa awali.

”Hadi sasa hatujapokea maombi yoyote ya kusogezwa mbele kwa mchezo huo, hivyo maandalizi yanaendelea kama kawaida na kila kitu kinakwenda kama kilivypangwa”Alisema Boimanda.

Ufafanuzi huo unakuja siku chache zilizopita kufuatia uvumi uliosambaa mitandaoni kuwa huenda Simba ingeomba kusogezwa mbele kwa mchezo huo kutokana na kuwa na mfululizo wa mechi za kimataifa dhidi ya Orland Pirates mnamo tarehe 14 na 24 hatua ya robo fainali.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA SIMBA SAFARI HII...NABI KAKUNA KICHWA WEEE...KISHA AKAGUNA NA KUSEMA HAYA...