Home Habari za michezo MANARA ASHINDWA KUFICHA ‘MAHABA YAKE KWA SIMBA’…AMFUATA PABLO HOTELINI..AMTAKIA USHINDI KESHO..

MANARA ASHINDWA KUFICHA ‘MAHABA YAKE KWA SIMBA’…AMFUATA PABLO HOTELINI..AMTAKIA USHINDI KESHO..


Msemaji wa Young Africans Haji Sunday Ramadhan Manara kwa mara ya kwanza amekutana na Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Franco Pablo Martin.

Haji amethibitisha kukutana na Kocha huyo kutoka nchini Hispania na kupiga picha ya pamoja wakiwa jijini Dar es salaam, huku akianika ukweli wa kukutana kwao jijini humo.

Manara amethibitisha hilo kwa kuweka picha ya pamoja waliopiga na Kocha Pablo, sambamba na kuandika ujumbe ambao mwisho alimtaja Kocha wa Young Africans Nasreeddin Nabi.

Manara ameandika: “Maeneo ya Sea Cliff Mchana huu,,nilipokutana na Kocha wa Simba Pablo,akiwa na Mkewe na Mtoto wao Mdogo, akaniita kunisalimia na tukaongea machache, huku akitukakia kheri kwenye mchezo wetu ujao wa ligi dhidi ya Azam na mm nikijibaraguza kumtakia kheri kesho.”

Sikuwahi kukutana nae before, kumbe zile Swaga zake za uwanjani ni temple tu ya mechi, very humble Guy and Gentleman.

Nilipenda tulipoagana aliponiambia msalimie Professor Nabil.

Fair Play of football 🙏🏻

Haji tangu alipoondoka Simba SC hakuwahi kupiga picha na Afisa yoyote wa Benchi la Ufundi la klabu hiyo na kuanika hadharani kama alivyofanya kwa Kocha Pablo.

SOMA NA HII  KUHUSU BANGO LA 5G LA YANGA....SIMBA WAAMUA KUCHUKUA HATUA HIZI MAPEMAA...