Home Habari za michezo MANARA AWAUMBUA WANAOMSHAMBULIA KUVAA JEZI YA ORLANDO…ADAI MKUDE MBONA ALIVAA..?

MANARA AWAUMBUA WANAOMSHAMBULIA KUVAA JEZI YA ORLANDO…ADAI MKUDE MBONA ALIVAA..?


Msemaji wa Yanga Haji Manara amesema sio yeye tu aliyevaa jezi ya Orlando Pirates, hadi Mchezaji wa Simba (aliyemuita fundi ) Jonas Mkude amevaa jezi hiyo.

Hivi karibuni Haji Manara amekutana na upinzani mkali baada ya kuvaa jezi hiyo kutoka kwa wachambuzi wa soka wakidai amefanya makosa kadhaa ikiwemo kuikosea heshima klabu yake ya Yanga.

Miongoni mwa wachambuzi aliyemshambulia vikali Manara ni pamoja na Jemedari Saidi wa kituo cha EFM, ambapo alidai kuwa kitendo cha Manara kuvaa jezi ya Orlando ni kuikosea heshima GSM,ambao ni wadhamini wa vifaa na jezi za Yanga pamoja na SportsPesa ambao ni wadhamini wakuu wa klabu hiyo.

Hii si mara ya kwanza kwa maofisa wa Yanga kuvaa jezi za timu kutoka Afrika Kusini kwani mwaka jana Injini Hers Saidi naye alivaa jezi ya Kaizer Chiefs mara baada ya kuifunga Simba kwenye mechi ya kwanza ya hatua ya robo fainal ya Klabu Bingwa Afrika nchini Afrika kusini.
SOMA NA HII  WAZAMBIA WAIFANYIA KITU MBAYA TANZANIA ....TWIGA STARS WABANWA MBAVU AFRIKA KUSINI...JESHIMA YAO YAPOTEA ...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here