Home Habari za michezo MASAU BWIRE NA RUVU YAKE WAIPELEKA YANGA KIGOMA…WADAI NI SUALA LA KIKANUNI….

MASAU BWIRE NA RUVU YAKE WAIPELEKA YANGA KIGOMA…WADAI NI SUALA LA KIKANUNI….


Timu ya soka ya Ruvu Shooting imetangaza mchezo wake wa marudiano Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Yanga utafanyika Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema leo Ijumaa kuwa, hatua hiyo inatokana na kupokea maombi kutoka kwa wadau wa mpira wa miguu mkoani humo.

“Pia ni suala la kikanuni. Kanuni ya tisa ya Ligi Kuu Tanzania Bara kifungu kidogo cha saba inaruhusu timu mwenyeji kuhamisha michezo yake miwili kwenda kwenye uwanja ambao hautumiki na timu ya Ligi Kuu.

“Pia tulipokea maombi kutoka mikoa mbalimbali kama vile Tabora, Ruvuma, Mwanza na Arusha, lakini tukakubaliana na maombi ya Kigoma kwa sababu tangu timu yetu ipande Ligi Kuu hatujawahi kwenda kucheza huko,” amesema Bwire.

Alisema ni matumaini yao kwamba mashabiki wa Kigoma na maeneo ya jirani watapata burudani ya kutosha katika mchezo huo utakaofanyika Mei 4, 2022.

SOMA NA HII  WAKATI WAKIJINDAA NA SINGIDA BIG STARS....MASUDI DJUMA KAJIPIGA PIGA KIFUANI ..KISHA KWA JEURI AKASEMA HAYA...