Home Habar za Usajili Simba IBENGE NA TIMU YAKE WATIBUA DILI LA ADEBAYOR KUTUA SIMBA…WAMWAGA MAMILIONI YA...

IBENGE NA TIMU YAKE WATIBUA DILI LA ADEBAYOR KUTUA SIMBA…WAMWAGA MAMILIONI YA PESA…


Mipango ya Simba kumnasa winga matata kutoka USGN ya Niger, Victoriesn Adebayor, huenda ikaingia mchanga,. Ukweli ni kwamba RS Berkane ya Morocco, wametia mkono kwenye usajili huo na kama mabosi wa Simba wasipokomaa huenda jamaa akapeperuka kama utani kwani Waarabu wako siriazi na wanaeka mkwanja wa maana ambao hata wewe huwezi kuuacha.

Simba ipo kwenye mazungumzo na nyota kadhaa akiwamo Moses Phiri wa Zanacco ya Zambia, Stephane Aziz Ki (Asec Mimosas), ambaye pia anawindwa na Yanga na Adebayor aliyekuwa kwa mkopo USGN.

Kwa nyakati tofauti Simba imefanya mazungumzo na Wakala wa Adebayor, mchezaji mwenyewe pamoja na viongozi wa USGN waliyomchukua kwa mkopo kutokea timu ya HB Koge ya Denmark,.

Taarifa za uhakika ni kwamba mabosi wa RS Berkane ya Kocha Florent Ibenge wamefanya mazungumzo na timu ya HB Koge inayommiliki Adebayor na upepo unaelekea upande wao kwani wamewekewa mzigo wa maana walio tayari kuutoa.

“Maslahi binafsi na mchezaji tayari wamekubaliana, kuna pesa nyingine USGN wanatakiwa kupata kutokana na usajili huu tupo tayari kuwapa na kilichobaki ni makubaliano na klabu yake tu ya HB Kobe,

“Tunafahamu Simba wanamhitaji na wamepiga hatua kwa kiasi fulani juu ya suala hili ila wanaweza kukwama kwenye mambo mawili pesa inayohitajika mchezaji apatikane ni nyingi,”kilidokeza chanzo chetu ndani ya Berkane.

SOMA NA HII  WABABE WA SIMBA WATUA YANGA...WATOA KAULI YA KIBABE MNOOO...