Home Azam FC MASKINI YA MUNGU PRINCE DUBE JAMANI…LIMEBAKI JINA NA HISTORIA TU…USIOMBE IKUKUTE…

MASKINI YA MUNGU PRINCE DUBE JAMANI…LIMEBAKI JINA NA HISTORIA TU…USIOMBE IKUKUTE…


PRINCE Dube, mshambuliaji aliyetupia bao moja kwenye ligi msimu huu, ambaye ni mchezaji wa mwisho kuifunga Yanga bao la ushindi, mambo kwake bado ni magumu kwa kuwa hajarudi kwenye ule ubora wake wa msimu uliopita.

Ikumbukwe kwamba mara ya mwisho Yanga kufungwa kwenye mechi ya ligi ilikuwa ni Aprili 25, 2021 Dube alifunga bao pekee Uwanja wa Mkapa. Leo Aprili 8 ni siku ya 349 kwa Yanga kutimiza bila kufungwa huku nyota Dube naye akishindwa kuivunja rekodi yake mwenyewe.

Juzi walipokutana Uwanja wa Azam Complex, Dube aliwekwa chini ya ulinzi wa ukuta wa Bakari Mwamnyeto na Dickosn Job ambao walikuwa wanakula naye sahani moja na alishuhudia timu ya Azam ikifungwa mabao 2-1.

Ndani ya dakika 90 ambazo alitumia, alipiga pasi 30 na alikokota mpira mara mbili na kuchezewa faulo mara 4, alicheza faulo mara mbili na aliotea mara moja ilikuwa dk ya 9.

Alipiga shuti moja ambalo halikulenga lango dk ya 8 na alipiga shuti lililolenga lango dk ya 9 lakini liliishia mikononi mwa kipa wa Yanga, Diarra Djigui. Bao pekee ambalo Dube alifunga msimu huu ilikuwa ni Machi 16, 2022 walipoichapa Namungo 2-1 wakiwa ugenini.

SOMA NA HII  CAF YAIPIGA RUNGU LA ADHABU SIMBA KWA KUFANYA "TAMBIKO LA KISHIRIKINA" UWANJANI....

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here