Home Habari za Yanga NTIBAZONKIZA AVUNJA UKIMYA YANGA…ADAI ANA DENI ZITO…AMTAJA MAYELE NA NABI…

NTIBAZONKIZA AVUNJA UKIMYA YANGA…ADAI ANA DENI ZITO…AMTAJA MAYELE NA NABI…


Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Saido Ntibazonkiza amevunja ukimya na kusema tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi wa Ligi Kuu imempa hamasa ya kujituma zaidi katika mechi zilizobaki, kwani anajiona ni kama mwenye deni kubwa.

Saido alisema tuzo hiyo ni deni kwa klabu yake, akisisitiza imemwongezea mzuka wa kupambana zaidi kuhakikisha timu yao inatwaa ubingwa na tuzo hiyo inarudi tena Jangwani kabla ya msimu kumalizika.

Kiungo huyo mwenye mabao sita na asisti tano, alishinda tuzo hiyo kwa Februari, huku straika wa timu hiyo, Fiston Mayele akishinda ile ya Januari sambamba na Kocha Nasreddine Nabi aliyetwaa tuzo ya Kocha Bora wa Februari.

Kwa mwezi uliopita, Clatous Chama wa Simba alitwaa tuzo ya Mchezaji Bora wakati Pablo Franco akishinda kwa upande wa Kocha Bora kwa mwezi huo.

Saido, Mayele na Nabi walizawadiwa Sh1 milioni kila mmoja na David Raymond kutoka kitengo cha Idara ya Masoko wa Benki ya NBC inayoidhamini Ligi Kuu.

“Ni faraja kubwa kushinda tuzo hii, sio mimi tu, hata kwa Fiston na Nabi ambaye ni kocha wetu, imeniongezea hamasa na kujiona napaswa kupambana zaidi ili rekodi hii kujirudia katika timu yetu na kutwaa ubingwa mwisho wa msimu,” alisema.

SOMA NA HII  KISA SIMBA MABOSI WA SOKA AFRIKA NA DUNIA KUTUA TZ...UWANJA WA MKAPA KUINGIZA MIL 80..