Home Habari za michezo PENATI YA KAPOMBE DHIDI YA WASAUZI YATOA SOMO LIGI KUU…MABEKI WAFUNGUKA WALICHONASA….

PENATI YA KAPOMBE DHIDI YA WASAUZI YATOA SOMO LIGI KUU…MABEKI WAFUNGUKA WALICHONASA….


Umahiri na ujasiri aliouonyesha beki wa Simba, Shomari Kapombe kupiga penalti muhimu ya bao pekee dhidi ya Orlando Pirates, umetoa somo kwa baadhi ya mabeki kujifunza kitu kwake.

Mbali na penalti ya juzi ya mechi ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwenye Uwanja wa Mkapa, ya kwanza alifunga dhidi ya ASEC Mimosas, akitupia bao la pili lililowarejesha mchezoni na kumaliza dakika 90 kwa ushindi wa mabao 3-1.

Beki wa Mtibwa Sugar, Ibrahim Ame alisema ugumu wa penalti alizopiga Kapombe CAF, ulitokana na Simba kupata matokeo ya ushindi na kama angekosa huenda timu isingefika hapo.

Adeyum Saleh, beki wa Geita Gold alimsifu akisema:

β€œPenalti kama zile zinahitaji kujiamini maana zinakuwa zimebeba hatima za furaha ya mashabiki ndiyo maana wengine wanazimia na wengine kupoteza maisha.”

SOMA NA HII  BAADA YA 'KUFURUSHWA' NA DODOMA JIJI...MBEYA KWANZA WAMUOKOA MAKATA..KUANZA KAZI LEO..