Home Habari za michezo UNAMKUMBUKA KAHATA..HUYU HAPA…KALA SHAVU TIMU YA POLISI KENYA…AFICHUA HAYA MAPYA…

UNAMKUMBUKA KAHATA..HUYU HAPA…KALA SHAVU TIMU YA POLISI KENYA…AFICHUA HAYA MAPYA…


MOJA kati ya viungo wabunifu kuwahi kutokea nchini Kenya Francis Kahata hana mpango wa kustaafu kabisa.

Licha ya kuwa ubora wa kiwango chake umeshuka mno kuliko alivyokuwa miaka ya nyuma, Kahata mwenye miaka 32 bado hajawazia kuachana na soka.

Kahata anasisitiza kuwa ni mapema mno kuanza kuwazia kustafu soka na hivyo ataendelea kupambana.

Staa huyo wa zamani kwenye timu ya taifa, anasema bado angali na ndoto ya kucheza soka majuu hii ikiwa ni miezi kadhaa tu toka aliposaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea Police FC.

Kiungo huyo aliyesifika kwa pasi zake na maujanja uwanjani miaka ya nyuma kidogo, ni miongoni mwa mastaa wazoefu waliosajiliwa na Police kuisaidia kutwaa ligi kuu msimu huu lakini hesabu hazijawaendea poa.

Kurejea kwake Kenya baada ya kucheza soka la kulipwa Tanzania, Ethiopia na Albania kuliwafanya wengi kusaidiki kuwa, safari yake  kwenye taaluma ya soka ndio inaelekea ukingoni.

“Bado sijakataa tamaa ya kucheza soka nje majuu. Mimi kujiunga n na Kenya Police msimu huu haimaanishi nawaza kustaafu kutoka kwenye soka hivi karibuni. Inawezekana ni mtazamo wa wengi ila hauko sahihi. Mimi bado sana kustaafu soka,” Kahata kafunguka.

Licha ya Kenya Police kuendelea kuhangaika na uzalishaji matokeo wakijikuta katika nafasi ya 11 kwa alama 28 baada ya mechi 24 zikiwa zimesalia mechi nane, Kahata ambaye naye amekuwa akihangaikia fomu yake, anaamini ana uwezo wa kuwabeba.

“Naamini kabisa tunaweza kumaliza msimu kwenye top 5 ukizingatia upana wa kikosi chetu na kiwango cha wachezaji tulionao. Tuna mchanganyiko wa chipukizi na wazoefu na hili linanipa matumaini makubwa kuwa tutafanikiwa katika hili,

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA MAYELE KUTAKIWA KAIZER CHIEF....NABI AFUNGUKA A-Z DILI ILIVYO NA UKWELI WA MAMBO...