Home Habari za michezo WAKATI WATU WAKIMUONA ‘CHENGA’ KWA VITUKO VYAKE…UKWELI NI KWAMBA HAKUNA SIMBA BILA...

WAKATI WATU WAKIMUONA ‘CHENGA’ KWA VITUKO VYAKE…UKWELI NI KWAMBA HAKUNA SIMBA BILA MORRISON..


KATIKA mechi 10 ambazo Simba imecheza kwenye michuano ya CAF msimu huu imefunga mabao 16 huku winga wao, Bernard Morrison ndiye mchezaji pekee aliyechangia idadi kubwa zaidi (saba), akifuatia Shomari Kapombe (matatu).

Morrison aliyeonyesha ukomavu CAF, anaongoza kwa asisti tano, huku akifunga mabao matatu na hiyo ilitokana na ujanja wake pamoja na wepesi wa kukabailiana na mabeki wa timu pinzani.

Mchezaji huyo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika alitoa asisti moja na upande wa Kombe la Shirikisho alitoa asisti tatu huku akifunga mabao matatu.

Kwenye ligi hiyo, Simba ilicheza mechi mbili dhidi ya Jwaneng Galaxy na walishinda jumla ya mabao matatu baada ya mchezo wa kwanza Simba kushinda 2-0 na kwenye mchezo wa marudiano alifungwa 3-1 na kuondolewa katika kombe hilo na kwenda kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika kuanzia hatua ya makundi.

Morrison alitoa asisti kwenye mchezo waliofungwa 3-1 huku Lary Bwalya akifunga bao la kufutia machozi.

Katika mchezo wa kwanza kwenye Shirikisho, Simba walianza na Red Arrows uliomalizika wakishinda 3-0, Morrison alifunga mabao mawili huku bao la tatu likifungwa na Meddie Kagere (asisti Morrison).

Morrison alisawazisha dhidi ya USGN (1-1) Simba ikiwa timu pekee kundi D kupata pointi ya ugenini.

Mchezaji huyu alikuja kuhusika tena katika ushindi wa 4-0 dhidi ya USGN akitoa asisti mbili na kuifanya Simba itinge hatua ya robo fainali ya Kombe hilo kibabe.

Kocha msaidizi wa Kagera Sugar, Ulimboka Mwakingwe alisema Morrison ana uwezo wa kuamua mechi ngumu na kuutafsiri mchezo unataka nini, jambo analoamini linamng’arisha mechi za kimataifa.

“Anajua anachokitaka uwanjani, akiamua kuwekeza nguvu zaidi kwenye kazi, atafanya makubwa zaidi ya hayo tunayomuona anafanya,” alisema.

Kauli hiyo iliungwa mkono na beki wa zamani wa timu hiyo, Godwin Aswile aliyesema alichokigundua kwa Morrison ana maamuzi ya kucheza kwa kiwango cha juu ama chini.

“Ana maamuzi ya nini afanye, nimemwona kwenye mechi ngumu ambazo Simba inahitaji matokeo, anapambana na kujitoa, mfano alitengeneza nafasi nyingi dhidi ya USGN alipoona anaowapa asisti wafunge hawafungi akaanza kujaribu kupiga mwenyewe, tafsiri yake alihitaji kuona wanapata mabao, hiyo ndio maana ya mchezaji mkubwa,” alisema.

SOMA NA HII  AFISA HABARI SIMBA AFUNGUKA ISHU YA YANGA KUMTAKA AENDE KWAO...AGUSI ISHU YA KUFUKUA MAFAILI...