Home Habari za michezo REFA ALIYESHTAKIWA KWA KUIBEBA SIMBA KWA MKAPA AULA KOMBE LA DUNIA….CAF WAZIBA...

REFA ALIYESHTAKIWA KWA KUIBEBA SIMBA KWA MKAPA AULA KOMBE LA DUNIA….CAF WAZIBA MASIKIO…


Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) limemtetua refa Jean Jacques Ndala Ngambo kwtika orodha ya awali ya waamuzi wa kati kwa ajili ya kuchezesha Fainali za Kombe la Dunia baadaye mwaka huu.

Refa huyo kutoka Jamhuri ya DR Congo alizua mjadala hivi karibuni baada ya RS Berkane ya Morocco kumlalamikia kuwa aliipendelea Simba katika mechi ya raundi ya nne ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu ambayo walipoteza kwa bao 1-0.

Hata hivyo malalamiko hayo yalitupiliwa mbali na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Caf) na siku chache baadaye refa huyo alipangwa kuchezesha mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia baina ya Misri na Senegal.

Orodha hiyo ya awali ya waamuzi nane wa kati kutoka Afrika imehusisha marefa waandamizi ambao wana historia na uzoefu mkubwa wa kuchezesha mechi kubwa na zenye ushindani wa hali ya juu.

Refa aliyezua mshangao katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) zilizofanyika Cameroon mwaka huu, Janny Sikazwe kutoka Zambia naye amejumuishwa katika orodha hiyo ambayo haina jina hata moja la refa kutoka nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (Cecafa).

Marefa nane wa kati kutoka Afrika walioteuliwa katika orodha ya awali ya kuchezesha Fainali za Kombe la Dunia ni Mustapha Ghorbal (Algeria), Redouane Jayed (Morocco), Bakary Gassama (Gambia), Bamlak Tessema (Ethiopia), Victor Gomez (Afrika Kusini), Janny Sikazwe (Zambia), Maguette N’ diaye (Senegal) na Jean Jacques Ndala Ngambo (DR Congo)

SOMA NA HII  FT: RUVU SHOOTING 0-4 SIMBA SC.....BOCCO AMJIBU MAYELE KIBABE....CHAMA SAWA NA MAJI TU...USIPOKUNYWA UTAYAOGA...