Home Burudani ILE ISHU YA MWAKINYO KUZICHAPA MAREKANI KUMBE IKO HIVI BANA…APOROMOKA UBORA WA...

ILE ISHU YA MWAKINYO KUZICHAPA MAREKANI KUMBE IKO HIVI BANA…APOROMOKA UBORA WA VIWANGO…


Licha ya kuporomoka kwa nafasi tatu kwenye ubora wa dunia, Menejimenti ya Hassan Mwakinyo imeeleza mipango ya bondia huyo kucheza nchini Marekani bado haijakamilika.

Mwakinyo yuko Marekani kwa wiki kadhaa ambako anajifua katika harakati za kucheza pambano la ubingwa wa WBA nchini humo.

Hata hivyo, akiwa kwenye harakati hizo, bondia huyo ameporomoka kwa nafasi tatu kwenye ubora kwa mujibu wa mtandao wa ngumi za kulipwa wa dunia (Boxrec).

Boxrec imemtaja bondia huyo namba moja nchini kuwa kwenye nafasi ya 17 kutoka ya 14 aliyokuwa awali kwenye uzani wa super welter duniani.

Mwakinyo ameporomoka kutokana na kutocheza muda mrefu, tangu Septemba 3, 2021 alipomchapa Julius Indonga kwa TKO na kutetea ubingwa wa Afrika (ABU) ambao pia alivuliwa hivi karibuni sababu hajacheza pambano jingine.

“Bado tuko kwenye mazungumzo na promosheni mbili, ambazo mojawapo ndiyo itamuandalia Mwakinyo pambano nchini Marekani,” alisema meneja wa bondia huyo, Huzeifa Huzeifa.

“Tunaangalia ofa zao, lakini pia na nafasi ya bondia wetu ya mbele, tuko kwenye majadiliano ya kuingia mkataba na kujiridhisha na mabondia watakaotuletea, japo hatuangalii sana bondia wetu atalipwa kiasi gani.

“Japo kulikuwa na changamoto chache kwa kuwa sisi sio wakazi wa kule, lakini mpaka sasa tuko kwenye hatua nzuri ya Mwakinyo kuingia mkataba wa kucheza pambano lake la 23,” alisema.

Mwakinyo kwa sasa ni bondia wa 17 kati ya 1882 duniani kwenye uzani wa welter unaoongozwa na Jermell Charlo wa Marekani, Brian Carlos Castano wa Argentina na Sebastan Fundora wa Marekani.

SOMA NA HII  RASMI....PHIRI AKABIDHIWA 'SHOW' ZAKE SIMBA...MBRAZILI AAMUA KUJILIPUA KUMJARIBU TENA...