Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA SIMBA…SENZO ALIPUA JAMBO YANGA…AMTAJA MAYELE…AFICHUA JAMBO LITAKAVYOISHA…

KUELEKEA MECHI NA SIMBA…SENZO ALIPUA JAMBO YANGA…AMTAJA MAYELE…AFICHUA JAMBO LITAKAVYOISHA…


YANGA ipo jijini Mwanza kwa ajili ya mechi mbili ngumu, lakini hapohapo wakapeleka salamu nzito kwa watani zao Simba watakaokutana nao Mei 28 jijini humo.

Yanga ambayo juzi usiku iliichapa Mbeya Kwanza mabao 4-0 katika Ligi Kuu Bara, watakuwa na dakika 90 za kwanza leo za ligi dhidi na Biashara United kisha mchezo wa pili dhidi ya Simba wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam.

Akizungumza, Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mazingisa alisema kuwa ushindi wao wa juzi ni salamu tosha kwa watani zao kwamba hawataki kuacha kitu msimu huu.

Senzo alisema wako Mwanza wakiwa kamili katika kila idara na baada ya kushindwa kufungana kwenye dakika 180 za ligi sasa wanataka kwenda kushinda mchezo huo.

Alisema kwa sasa timu yao imerudi katika uborana amezungumza na wachezaji walioonyesha kiu ya ushindi katika mechi zote mbili za mkoani humo..

“Tunawaheshimu Simba lakini mchezo ujao tuna dhamira na nguvu kubwa ya kushinda hukohuko Mwanza, nafikiri mnafahamu nguvu yetu tukiwa ndani ya jiji hili,” alisema.

Senzo alisema jeuri nyingine ya kuelekea mchezo huo ni kurudisha hali ya kujiamini kwa mshambuliaji wao Fiston Mayele ambaye juzi alifunga bao lake la 13 baada ya kukumbwa na ukame mechi nne.

“Tunaposema timu imerudi mnaona Mayele amerudi katika ubora. Hii ni hatua ambayo kila Mwanayanga alikuwa na kiu nayo, anapofunga Mayele na timu ikashinda ushindi unakuwa na utamu zaidi.”

“Hii itamrudishia hali ya kujiamini ambayo ilipotea kwa hivi karibuni, Yanga tunafurahi lakini nafahamu timu zingine zinaogopa hili.”

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA TP MAZEMBE....HIZI HAPA DK 270 ZA YANGA KUSUKA AU KUNYOA CAF...