Home Habari za michezo KUPANDA LIGI KUU MSIMU UJAO….DTB YATIA ‘MCHANGA KITUMBUA’ CHA IHEFU…’YAIGONGA CHA NGURUWE...

KUPANDA LIGI KUU MSIMU UJAO….DTB YATIA ‘MCHANGA KITUMBUA’ CHA IHEFU…’YAIGONGA CHA NGURUWE CHWAAAW’…


MECHI ya heshima baina ya DTB na Ihefu, imepigwa Uwanja wa Uhuru, ambapo bingwa wa Ligi Championship anakabidhiwa taji.

Ihefu inakabidhiwa taji hilo, ikiwa imechapwa bao 1-0 dhidi ya DTB.

Dakika 45 za kipindi cha kwanza, wachezaji wa timu zote mbili waliingia kwa kuviziana hadi dakika ya 15 mshambuliji Amisi Tambwe alipolinyanyua benchi la DTB.

Mpira ulianza kwa kupooza huku DTB wao wakionyesha kuhitaji mabao zaidi kutokana na kucheza kwa mipango tofauti na wapinzani wao.

Dakika ya 19 Ihefu ilijaribu shambuliji la mbali ambalo lilipanguliwa na Owen Chaima na kuzaa kona ambayo haikuwa na madhara langoni mwa DTB kutokana na umakini wa mabeki.

Pamoja na kutanguliwa kwa bao moja Ihefu walikosa mipango na kuwaacha DTB wautawale mchezo hadi kipyenga Cha mwamuzi kinapulizwa walitoka kichwa chini na kuwaacha wenzao wakiongoza kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili Ihefu iliingia kwa kuwapa presha DTB na kuliandama mara kwa mara lango la wapinzani wao lakini safu yao ya ushambuliaji ilikosa umakini na kushindwa kutumia nafasi za wazi walizozitengeneza.

Nahodha wa Ihefu, Joseph Kinyozi amekosa umakini ndani ya box baada ya kutengenezewa nafasi mbili ambazo zote alishindwa kukwambisha nyavuni.

Ihefu ilitawala mchezo kipindi cha pili na kumpa wakati mgumu kipa Chaima ambaye nyota yake iling’ara kutokana na kupigiwa pasi nyepesi ambazo zilikowa kawaida kwake kuziokoa.

 Pamoja na kupata nafasi nyingi Ihefu kucheza vizuri kipindi cha pili na kutengeneza nafasi zaidi ya tatu walishindwa kuzitumia Hadi kipyenga Cha mwisho kinapulizwa.

SOMA NA HII  PACOME AJITISHWA 'ZIGO' LA LIGI YA MABINGWA KWA YANGA...