Habari za michezo

CAF WAIPIGA ‘JEKI KIMTINDO’ TAIFA STARS KUFUZU MASHINDANO YA CHAN….WASHINDWE WAO TU SASA…

admin May 25, 2022 2:13 am


Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeandaliwa mazingira mazuri ya kufuzu fainali zijazo za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN) baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuongeza idadi ya timu shiriki kutoka 16.

Uamuzi wa kuongeza idadi ya timu katika mashindano hayo umefanywa na kamati ya utendaji ya CAF iliyoketi hivi karibuni huko Cairo, Misri.

Taarifa iliyotumwa na mkurugenzi wa mashindano wa CAF, Samson Adam kwenda kwa mashirikisho na vyama vya soka vya nchi wanachama wa shirikisho hilo, imefafanua nyongeza ya idadi ya timu za kufuzu mashindano hayo kwa kila kanda ya soka.

“Tunakujulisha kwamba kamati ya utendaji ya CAF imepitisha ongezeko la timu kwenye awamu ijayo ya mashindano ya CHAN hadi timu 18,” ilifafanua sehemu ya taarifa hiyo ya CAF.

Kwa mujibu wa ongezeko hilo, kila kanda iliyo chini ya CAF itawakilishwa na timu tatu katika mashindano hayo yatakayofanyika mwakani huko Algeria.

Kwa ongezeko hilo, Kanda ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) itawakilishwa na timu tatu badala ya mbili kama ilivyokuwa hapo awali.

Awamu iliyopita mashindano hayo yalipofanyika Cameroon, CECAFA iliwakilishwa na Taifa Stars na Uganda.

KUELEKEA MECHI YA DABI MWANZA….MWAKALEBELA ASHTUKIA JANJA JANJA YA SIMBA…AIFANYIA UMAFIA WA HATARI… WAMOROCCO WAKUBALI KUIPA SIMBA BEKI KITASA CHA KAZI…YANGA WAMUINGIZA ‘CHAKA’ PABLO…NABI AKESHA NA MAYELE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply