Habari za michezo

HUKU HOMA YA PAMBANO LA WATANI LIKIZIDI KUPANDA….YANGA WAIKIMBIA SIMBA MWANZA…ISHU NZIMA IKO HIVI…

admin May 25, 2022 1:59 am


VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wenye pointi 64 wanatarajiwa kuweka kambi mkoani Shinyanga kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba.

Huu ni mchezo wa hatua ya nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho ambapo mabingwa watetezi ni Simba walitwaa taji hilo walipocheza fainali na Yanga, Uwanja wa Lake Tanganyika kwa ushindi wa bao 1-0.

Juzi,  Yanga ilikuwa na kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Biashara United na mchezo huo ulikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1, Uwanja wa CCM Kirumba.

Na jana kikosi cha Yanga kimeanza safari kuelekea Shinyanga ambapo kitaweka kambi kwa ajili ya mchezo wao ujao dhidi ya Simba.

Cedrick Kaze,Kocha Msaidizi wa Yanga amesema kuwa wanatambua mchezo wao ujao utakuwa ni mgumu ila watajitahidi kusaka ushindi.

“Tunajua kwamba mchezo wetu ujao utwakuwa ni wa nusu fainali dhidi ya Simba, tunawaheshimu wapinzani wetu na tutafanya maandalizi vizuri,”.

KUELEKEA MECHI NA YANGA….PABLO AAMBIWA LAZIMA ASHINDE…KAPOMBE ARUDI MAZIMA…MANULA MHHHH… ZIKIWA ZIMESALIA SIKU TATU KABLA YA KUKIPIGA NA YANGA…PABLO ALIA MAMBO MAGUMU SIMBA…HAJUI AFANYE NINI KUISAIDIA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply