Bodi ya Premier League imethibitisha mapendekezo ya kuuzwa kwa klabu ya Chelsea kwa Todd Boehly na washirika wake kama ilivyotangazwa jana jioni kwenye ligi hiyo.
Todd Boehly anayemiliki klabu ya Los Angeles Dodgers na washirika wake, wamekubali kulipa kiasi cha ยฃ4.25 bilioni kuinunua klabu hiyo kutoka kwa Roman Abramovich ambaye amekuwa akiimiliki kwa miaka 19 sasa.
Waraka wa Premier League uliotoka jana jioni unasomeka โ Bodi ya Premier League leo imethibitisha mapendekezo ya kuinunua klabu ya chelsea kwenda kwa Todd Boehly/Clearlake na washirika wake.
โMalipo yanabaki chini ya serikali ambao wanatoa kibali cha mauzo na kujiridhisha maridhiano ya mwisho hadi hatua ya malipo.โ